Msimu wa 2024/25 wa CAF Champions League umeanza na mashabiki wa soka kote barani Afrika wanasherehekea makundi mapya yanayoundwa. Mashindano haya ni mojawapo ya matukio makubwa zaidi katika soka la Afrika, yakileta pamoja klabu bora kutoka nchi mbalimbali. Mchakato wa kupanga makundi ya CAF champion league klabu bingwa utaanza Oktoba, 7 2024 baadhi ya timu zishaanza kufanya maandalizi ya kujiandaa na michuano hiyo.
Muundo wa Mashindano
CAF Champions League ina timu 16 zinazoshiriki kwenye hatua ya makundi, zikigawanywa katika makundi manne ya timu nne kila moja. Timu zinazofanya vizuri katika kila kundi zinafuzu kwa hatua ya robo fainali. Msimu huu, kuna matumaini makubwa kutoka kwa klabu mbalimbali, huku baadhi zikitarajiwa kufanya vizuri zaidi kuliko mwaka jana.
[SOMA PIA: Makundi ya shirikisho CAF]
Tazama hapa Makundi ya CAF Champions League 2024/25
Yafuatayo makundi ya CAF Champion league:
KUNDI A
- TP Mazembe
- Young Africans
- Al Hilal SC
- MC Alger
KUNDI B
- Mamelod Sundown
- Raja CA
- ASFAR Club
- AS Maniema Union
KUNDI C
- Al Ahly
- CR Belouizdad
- Orlando Pirates
- Stade d’Abidjan
KUNDI D
- Esperence De Tunisia
- Pyramids FC
- GD Sagrada Esperança
- Djoliba AC de Bamako
CAF Champions League 2024/25 inatoa fursa nzuri kwa timu na wachezaji kuonyesha uwezo wao katika kiwango cha juu zaidi. Ni wakati wa kushuhudia vipaji vya kipekee na mchezo wa soka wa kusisimua. Mashabiki wanapaswa kujiandaa kwa msimu wa kipekee wa mashindano haya na kuungana na klabu zao katika safari hii ya kutafuta ubingwa wa Afrika.