MATANGAZO YA KAZI
BOFYA HAPA
Katika makala hii fupi nitakuelekeza Jinsi ya Kuongeza Salio Kwenye N-Card kupitia M-Pesa. N card imeanza kutumika hapa Tanzania kwa wavukaji wa vivuko vya pantoni na mashabiki wa mpira wanaoenda kuangalia mpira viwanjani.
Watu wengi wanapata shida jinsi ya kuongeza salio kwenye N-card na hii kupelekea kuwepo na usumbufu wa kufika kwa mawakala na kuongeza salio, kuongeza mwenyewe salio kupitia M-pesa kutasaidia kuepusha umbufu huu na kupanga foleni kupoteza muda
Hatua Jinsi ya Kuongeza Salio Kwenye N-Card kupitia M-Pesa
Ikiwa unahitaji kuongeza salio kwenye N-card kupitia M-pesa tafadhari fata hatua zifuatazo:
- Piga *150*00#
- Chagua 4 “Lipa Bill”
- Chagua 4 “Namba ya Kampuni”
- Weka Namba ya Kampuni “009009”
- Weka Kumbukumbu Namba “Namba ya N-Card”
- Weka Kiasi
- Weka Namba ya Siri
- Thibitisha Muamala
Hadi hapo utakuwa umehafanikisha kuongeza salio kwenye N-card kupitia Mtandao wa M-pesa na unaweza kuendelea kutumia.