TCU imetangaza kukamilika wka udahili awamu ya pili na baadhi ya wanafunzi kuchaguliwa baadhi ya vyuo na kutakiwa vyuo zaidi ya kimoja na kutakiwa kuthibitisha, Ivo ivo Tum ya vyuo vikuu imetangaza kufungua awamu ya tatu ya Udahili kwa wanafunzi waliokosa nafasi kwa awamu mbili zilizopita.
TCU yathibitisha kufungua awamu ya tatu ya Udahili mwaka 2024/25
Baada ya kukamilika kwa awamu zote mbili za udahili, Tume imepokea maombi ya kuongeza muda wa kutuma maombi ya udahili kutoka kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), baadhi ya waombaji ambao hawakufanikiwa kupata udahili katika awamu zilizopita na pia vyuo ambavyo bado vina nafasi vimeomba vipewe muda kuendelea kudahili.
Hivyo, Tume imeongeza muda wa udahili kwa kufungua Awamu ya Tatu na ya mwisho ya udahili itakayoanza tarehe 05 hadi 09 Oktoba, 2024. Tume inawaasa waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi ya udahili au hawakuweza kupata nafasi ya kudahiliwa katika Awamu ya Pili kutokana na sababu mbalimbali, watumie fursa hii vizuri kwa kutuma maombi yao ya udahili kwenye vyuo wanavyovipenda.
Aidha, Tume inaelekeza Vyuo vya Elimu ya Juu nchini kuendelea kutangaza programu ambazo bado zina nafasi. Waombaji udahili na vyuo wanapaswa kuzingatia utaratibu wa udahili wa Awamu ya Tatu.
Mapendekezo: